Video · Angalia jinsi ilivyo rahisi kuotomatisha mchakato wa kutazama folda ili kubaini faili mpya. Wakati faili mpya inaonekana katika folda inayofuatiliwa, inaweza kunakiliwa, kutumwa kupitia barua pepe, kupakiwa kwenye seva ya FTP, kuchapishwa, kuchakatwa na programu ya mshirika mwingine, na mengineyo.
Majukumu ya kiotomatiki yanaweza kuanzishwa haraka sana. Hamna ujuzi wa kuandika misimbo ya programu unaotakiwa. Elekeza tu na ubofye ili kuanzisha Jukumu lako la kwanza la kiotomatiki!
Kiolesura maizi chenye zana za kubuni Majukumu na Vielelezo vya mipangilio kitakuelekeza katika mchakato wa kusanifu Jukumu bila kuhitaji ujuzi wa kuandika hati au mafunzo ya utangulizi. Ni rahisi kuotomatisha kitu chochote na mahali popote ukitumia mfumo huu wa kuotomatisha usiohitaji misimbo.
Utangulizi
- Umechoshwa na kazi za kujirudia?
- Ungependa kuotomatisha michakato ya kutuma, kunakili, kupakia na kuchapisha ankara zinazozalishwa kiotomatiki?
- Febooti Automation Workshop inaweza kukusaidia!
Kitazama Faili na Folda
- Kwanza, bofya kitufe cha "Jukumu Jipya" katika kidirisha cha programu kuu kisha uchague "Kitazama Faili na Folda" kutoka kwenye orodha ya vichochezi.
- Halafu, bainisha folda ambako ankara zitaandaliwa, nenda kwenye kichupo cha Masharti kisha uchague "Kutazama faili mapya".
- Kichochezi kiko tayari!
Nakili faili kwenye eneo la kuhifadhi
- Hebu sasa tuongeze vitendo vitakavyotekelezwa na jukumu.
- Automation Workshop inaruhusu zaidi ya vitendo 100 tofauti!
- Katika tukio hili, tungependa kuwasilisha nakala kwa eneo la kuhifadhi.
- Ili kunakili ankara ambayo tumepata, tumia Variable Wizard, chagua Kichochezi ulichobuni awali, na kisha weka eneo la kuhifadhi kwenye seva ya hifadhi.
Otomatisha barua pepe
- Sasa unahitaji kuweka Kitendo ambacho kinatuma barua pepe kiotomatiki pamoja na faili kwa: idara ya Mauzo.
- Andaa kiolezo cha barua pepe, kisha ubofye kitufe cha Variable Wizard, na uchague "kiambatisho".
Pakia faili kwenye seva
- Unaweza kuongeza vitendo vingi kwenye Jukumu.
- Kwa mfano, kuna Kitendo cha Kupakia Faili, kinachokuruhusu kupakia faili kwa mshirika wako wa biashara wa Seva ya FTP katika eneo tofauti.
- Tumia Variable Wizard, chagua Kichochezi tulichobuni awali, na uweke njia kwenye seva.
- Kisha, weka anwani na vitambulisho vya mtumiaji wa seva yako.
Otomatisha ufunguaji wa programu
- Kitendo kingine muhimu kinaruhusu programu ya mshirika mwingine kuchakata faili.
- Bofya "Washa Programu" na uweke njia ya programu.
Chapisha faili kiotomatiki
- Hatua ya mwisho ni kuchapisha ankara kiotomatiki.
- Ili uchapishe faili, weka Kitendo cha "Chapisha Faili", na utumie tu Variable Wizard.
Muhtasari
- Weka jina la jukumu, na ukamilishe kuandaa.
- Umemaliza! Jukumu limeanza kazi.
- Sasa, baada ya ankara mpya kufikia folda inayofuatiliwa, itanakiliwa kiotomatiki kwenye kompyuta nyingine, itatumwa kwa idara ya Mauzo, kupakiwa kwa seva ya FTP, kuzinduliwa kwa kutumia programu mahususi na kuchapishwa.
Inapatikana kote duniani
Kiratibu cha kina cha kazi—Automation Workshop hufanya kazi vyema katika matoleo yote ya kisasa ya biti 32 na 64 ya Microsoft Windows: Windows 10 · Windows 11 · Server 2016 · Server 2019 · Server 2022.
Matoleo ya zamani ya Windows (kama vile Windows 8 na Server 2012) hayatumiki "rasmi" lakini bado yanapaswa kufanya kazi vizuri. Usanifu wa Windows unabadilika na programu zetu zimebuniwa kufanya kazi na matoleo ya zamani na ya kisasa.