Maelfu ya watumiaji duniani kote tayari wanatumia zana ya kiotomatiki ya kuratibu kazi inayoitwa Automation Workshop. Bidhaa zetu hutumiwa popote kuotomatisha majukumu kwenye mifumo ya uendeshaji ya Windows. Tunabuni programu ambayo ni rahisi kutumia, na tunatoa huduma bora ya usaidizi. Febooti, Ltd. ni mojawapo ya kampuni bora za kuotomatisha programu nchini Latvia.
Kuotomatisha kazi za IT kunawaruhusu wafanyakazi kulenga majukumu yenye thamani ya juu, hali inayosababisha kupungua kwa gharama ya IT. Kuotomatisha pia kunasaidia kuimarisha ubora wa usimamizi wa IT na majukumu ya kudhibiti faili. Upakuaji wa jaribio lisilolipishwa unapatikana, na kuna mpango nyumbufu zaidi wa diskaunti ukinunua kwa wingi.
Automation Workshop
Huduma ya Automation Workshop ni zana ya kuratibu kazi ambayo inatekelezwa na studio ya kuotomatisha yenye kiolesura cha kuotomatisha maizi. Si lazima uwe na ujuzi wa kusanidi programu ili kuanzisha kazi zilizoratibiwa kulingana na tukio ukitumia teknolojia mahiri ya kuotomatisha—Vichochezi, Vitendo, Variable Wizard.
Kwa kuunganisha kiolesura maizi na ubainishaji anuwai wa vigezo, Automation Workshop inaruhusu kubuni Majukumu yenye mfano wa hati. Hivyo, bila kuhitaji uzoefu wa kuandika misimbo, una zana zinazoweza kuunganisha kiotomatiki michakato isiyounganishwa (yaani, iliyounganishwa na mtumiaji).
Otomatisha mahali popote na kila kitu ukitumia Kiratibu mahiri cha Kazi Vichochezi, faili maizi na vitazama folda za mbali, au vichochezi vya kuwasha mfumo. Vichochezi hivi vinaweza kuunganishwa kwa njia nyumbufu kwenye zaidi ya Vitendo 100 vya kuotomatisha kazi huruhusu kubuni majukumu ya kiotomatiki ya kazi kama vile shughuli za faili na folda, kubana faili kupitia matumizi ya zana ya kuhifadhi ya Windows au Linux, kupakia au kupakua faili kutoka seva salama za FTP au hata wingu.
Automation Workshop inajumuisha vipengele muhimu vya kudhibiti, kufuatilia, kuripoti na kuhifadhi ambavyo mtumiaji anaweza kutumia kutambua kimahususi michakato na matatizo na kuarifiwa kuhusu vitendo husika vya mfumo.
Inapatikana kote duniani
Matoleo yetu ya programu hufanya kazi vyema katika matoleo yote ya kisasa ya biti 32 na 64 ya Microsoft Windows: Windows 10 · Windows 11 · Server 2016 · Server 2019 · Server 2022.
Matoleo ya zamani ya Windows (kama vile Windows 8 na Server 2012) hayatumiki "rasmi" lakini bado yanapaswa kufanya kazi vizuri. Usanifu wa Windows unabadilika na programu zetu zimebuniwa kufanya kazi na matoleo ya zamani na ya kisasa.
Command Line Email
Ukiwa na Command Line Email, unaweza kutuma jumbe za kawaida za maandishi na jumbe changamano za muundo wa HTML, kuambatisha faili, hati na picha kwenye barua pepe, na kutuma barua pepe kutoka kwa Majukumu Yaliyoratibiwa, hati za CGI au programu yoyote inayoweza kutekeleza amri za nje. Amri zinazojifafanua za barua pepe zilizo na majina rahisi kukumbukwa zimejumuishwa.
Vipengele mahiri vya programu hii vinaruhusu kutumia vigezo kutoka kwa faili ya maandishi, kusimba maandishi ya ujumbe (Unicode, UTF-8, nk.), kutumia usimbaji wa MIME (Multipurpose Internet Mail Extensions), kutumia mbinu mbalimbali za uthibitishaji, kama vile AUTH PLAIN, LOGIN, NTLM, CRAM-MD5, na kutambua kiotomatiki, kuweka kipindi salama cha mawasiliano na seva ya SMTP kwa kutumia vipengele salama vya SSL au STARTTLS, na mengiyo…
Programu ya bure
Moduli huru za programu za bure zinazopatikana kwa urahisi zimetolewa kupitia ujumuishaji laini katika mfumo wa uendeshaji wa Windows. Upakiaji na upakuaji nyumbufu, una usaidizi unaolingana na muktadha.
- Hex Editor · angalia na ubadilishe faili katika hali za ASCII na HEX.
- Hash & CRC · kuchanganua usahihi wa faili, kama vile CRC32, MD5, na SHA-1.